Jumatano , 13th Nov , 2024

Kocha aliyeondoka kikosi cha mpira wa miguu kinachomilikiwa na Halmashauri ya Manispaa Wilaya ya  Kindoni Abdihamid Moalin kwa mujibu wa taarifa zisizo rasmi inasemekana akaibukia kwenye timu ya Yanga SC yenye makao yake makuu mtaa wa Twiga na Jangwani Karikaoo Dar es salaam.

Moalin alijiunga na KMC FC kutokea Azam FC alikofukuzwa kazi Augosti 29 2022.Raia huyo wa Marekani alitoa sababu tano zilizomfanya kuondoka KMC FC ikiwa bado mapema mzunguko wa kwanza wa ligi kuu Tanzania bara kutokana na kushindwa kuvumilia mazingira ya kazi kwenye kikosi hiko.

Kikosi cha Yanga SC kinahusishwa na kumshawishi kujiunga nao ili kwenda kuchukua nafasi ya Kocha wake msaidizi ambaye inasemekana atafukuzwa kazi muda wowote kwenye kikosi hiko mabingwa watetezi wa ligi ya Tanzania bara wa 2023-2024.Sababu yake kubwa ya kuondoka Manispaa ya Kinondoni ilikuwa ni kupangiwa kikosi na Viongozi wake pamoja na kucheleweshea mshahara wake.

Endapo kocha huyo mwenye umri wa miaka 35 atafanikiwa kujiunga na Yanga atafanikiwa kuweza kutengeneza vizuri zaidi CV yake kutokana na ukubwa wa timu ya Wananchi kwa soka la ndani Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Taarifa zinazoendelea kutoka kwenye vyanzo mbalimbali vya havari Tanzania zinatanabaisha juu ya uwezekano mkubwa wa Moalin kujiunga na kikosi cha Wanajangwani kuwa Mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo ambapo majukumu yake yatakuhusu kusimamia maenedeleo ya soka la Vijana na Wanawake,Kimarisha nidhamu kwenye timu zote pamoja na kulinda viwango vya Wachezaji wa timu hiyo.

Nafasi ya Ukurugenzi wa ufundi kwa Tanzania ni ngeni haijazoeleka na timu zetu za mpira wa miguu ila ni noja kati ya nafasi ambayo muhimu sana kwa uendeshaji wa timu kisasa.Kazi yake ikiwa ni kutengeneza na kusimamia falsafa ya timu, kusimamia uzalishaji wa Wachezaji wapya kupitia timu za Vijana kuajiri na kufukuza Makocha pale inapoonekana kushindwa kufikia malengo ya timu.

Huu utakuwa muendelezo wa Uongozi wa mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu Tanzania bara kuajiri kaumini na kuajiri Vijana kuunda safu mbalimbali za uongozi wa timu hiyo kuanzia Rais wa klabu na idara nyingine.Moalini Mmarekani mwenye asili ya Somalia anasifika kwa uwezo wake mkubwa wa kufundisha na kupenda mpira mzuri anatarajiwa  kufanya kazi nzuri endapo ataajiriwa na Yanga SC kutokana na mafanikio ya klabu hiyo na mpira unaochezwa kwasasa.