
Jeshi la Polisi limesema kwamba, limeanza uchunguzi wa tuhuma zilizo tolewa na Augustino Polepole kuwa, ndugu yao Humphrey Polepole ametekwa, jalada la uchunguzi lilifunguliwa jana hiyo hiyo.
Taarifa iliyotolewa leo Oktoba 7na jeshi la polisi ikirejerea taarifa ya jana Oktoba 6,2025, imedokeza kuwa pamoja na kukusanya taarifa mbalimbali, Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta Augustino Polepole ili aweze kutoa ushirikiano na kutoa maelezo yake na uthibitisho wa shutuma alizotoa.
Kwa mujibu wa taarifa ya polisi ikinukuu tuhuma za Augustino Polepole, Afisa wa Jeshi la Polisi alihusika katika tukio la utekaji wa Humprey katika taarifa iliyosambaa katika mitandao ya kijamii.
Aidha, Jeshi la polisi limesema kuwa jambo hilo linaenda sambamba na uthibitisho kuwa Humphrey Polepole alikuwa ni mpangaji ama mkazi wa nyumba aliyodai kuwa utekaji ulifanyika.