Amis Tambwe wa Yanga akiwakimbiza mabeki wa Ruvu Shooting
Ruvu Shooting ndiyo waliotangulia kuziona nyavu za Yanga katika dakika ya 7 kupitia kwa kiungo wake Ibrahim Musa ambaye alipata mpira kutoka upande wa kushoto kwa Yanga na kupiga shuti kali ambalo lilimshinda kipa wa Yanga.
Dakika ya 31 Yanga ilipata bao la kusawazisha kupitia kwa Simon Msuva aliyepokea pasi kutoka kwa Niyonzima mara baada ya mabeki wa Ruvu kujichanganya.
Kipindi cha kwanza kilikamilika huku timu zote zikienda mapumziko zikiwa sare ya bao 1-1.
Dakika ya kwanza ya kipindi cha pili cha mchezo Kocha Mkuu wa Yanga Hans van Pluijm anaondolewa kwenye benchi kwa kadi nyekundu kutokana na kupishana kauli na mwamuzi ambapo Kocha msaidizi Juma Mwambusi alishika kazi ya kuongoza kikosi katika mchezo huo.
Dakika ya 56 Yanga walipata bao la pili kupitia kwa Haruna Niyonzima ambaye alipata mpira kutoka kwa Ngoma ambaye aliubabatiza mpira kisha akampa pasi Niyonzima akapiga shuti na kujaa wavuni.
Dakika ya 74 Ruvu walifanya shambulizi lakini kipa wa Yanga, Kakolanya akaudaka.
Yanga na Ruvu Shooting imemaliza mzunguiko wa kwanza mara baada ya mchezo huo huku Yanga ikiwa nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi kwa kuwa na pointi 33 nyuma ya Simba ambayo inaongoza ligi ikiwa na pointi 35.