Yanga imekwenda Ethiopia tayari kwa mchezo wake wa marudiano wa mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika Jumatano ijayo dhidi ya wenyeji, Wolaita Dicha.
Wachezaji waliosafiri ni Makipa Youthe Rostand na Beno Kakolanya. Mabeki Hassan Kessy, Juma Abdul, Mwinyi Haji Mngwali, Gardiel Michael, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Kelvin Yondan na Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavario.
Viungo ni Papy Tshishimbi, Yussuf Mhilu, Raphael Daudi, Pius Buswita, Geoffrey Mwashiuya, Said Juma ‘Makapu’, Juma Mahadhi na Emmanuel Martin wakati washambuliaji ni Obrey Chirwa, Yohana Mkomola na Thabani Kamusoko.
Mchezo huo utapigwa kwenye Uwanja wa Hawassa mjini Hawassa na Yanga itakuwa na jukumu la kulinda ushindi wake wa 2-0 ilioupata kwenye mchezo wa kwanza uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Jumamosi iliyopita.