Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Klabu ya Simba Zacharia Hans-Pope amesema, walishaongea na Yanga wakati wanamsajili Kessy kuwa yupo ndani ya mkataba na Simba na walitakiwa kupata barua ambayo itathibitisha kuwa wameshaachana na Kessy lakini Yanga walikataa.
Pope amesema, ukitazama katika kanuni zinaonyesha wazi kuhusu suala la kumchukua mchezaji kabla mkataba wake haujaisha na wao hawakuvunja mkataba na Kessy bali walimpa adhabu lakini mkataba wake ulikua unaendelea.
Pope amesema, japo Yanga walipata leseni ya Shirikisho la Soka barani Afrika lakini bado katika hati ya uhamisho ya mchezaji TMS inaonyesha Kessy ni mchezaji wa Simba na wakaelezwa kuwa inatakiwa barua ili kuthibitisha kuwa ni kweli Kessy ameshamaliza Simba na sasa yupo Yanga.
Pope amesema, Yanga walifika ofisini kuomba barua siku ya jumamosi ya June 18 jioni ambayo hapo awali walikataa na ilikuwa vigumu kuwapa kwa wakati huo.
Pope amesema, iwapo Yanga watataka kumtumia Kessy itabidi wasubiri kipindi cha pingamizi za usajili kikishakamilika ndipo itasoma kwenye TMS kuwa ni mchezaji halali wa Yanga.
Pope amesema, kama Yanga wanataka kumtumia sasa hivi inabidi wawe wapole na wafuate sheria na ushauri na kama wakikataa wasubiri mpaka usajili ukamilike.

