Jumanne , 8th Apr , 2014

Michuano ya Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara inaendelea kesho (09 April 2014) kwa michezo miwili huku timu za Azam na Yanga ambazo zipo nafasi mbili za juu zikiendelea kuchuana

Kikosi Cha Yanga

Michuano ya Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara inaendelea kesho (09 April 2014) kwa michezo miwili huku timu za Azam na Yanga ambazo zipo nafasi mbili za juu zikiendelea kuchuana

Azam itakuwa mgeni wa Ruvu Shooting katika mechi itakayochezwa kwenye Uwanja wa Mabatini uliopo Mlandizi mkoani Pwani. Nayo Yanga itakuwa mwenyeji wa Kagera Sugar katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Kuelekea mchezo huo afisa habari wa Yanga Baraka Kizuguto amesema timu iko katika morali ya hali ya juu na wanatambua umuhimu wa mchezo huo na hivyo wamejipanga kuhakikisha wanaibuka na ushindi.