Yacouba Sogne akishangilia bao dhidi ya Biashara United
Bao pekee la Yanga kwenye mchezo huo limefungwa na Yacouba Sogne dakika ya 22 ya mchezo baada ya kupokea pasi ya upendo kutoka kwa kiungo mshambuliaji Feisal Salum ‘Fei Toto’. Mara ya mwisho Yanga kucheza fainali ya michuano hii ilikuwa msimu wa 2015-16 ambapo waliibuka mabingwa kwa kuifunga Azam FC, mabao 3-1.
Kwenye mchezo wa fainali timu ya Wananchi watacheza na mshindi wa mchezo wa nusu fainali ya Pili itakayo chezwa kesho Juni 25, 2021, huko Songea mkuani Ruvuma kwenye uwanja wa Majimaji ambapo Mabingwa watetezi Simba Sc watakuwa wakicheza na Azam FC.
Mchezo wa fainali ya michuano hii msimu huu utachezwa uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma


