Alhamisi , 23rd Apr , 2015

Chama cha mchezo wa WUSHU Tanzania TWA kesho kinatarajia kufanya mchujo ili kupata wachezaji watakaokwenda China kuhudhuria mafunzo ya mchezo huo.

Akizungumza na East Africa Radio, Katibu mkuu wa TWA, Gola Kapipi amesema wachezaji watakaohusika kwenye mchujo huo ni mikoa iliyoleta wachezaji ambao ni mikoa ya Dar es salaam, Morogoro na Tanga.

Kapipi amesema jumla ya wachezaji wapo nane ambapo mchujo huo utafanyika na kubaki watano ambao watakwenda nchini China.

Kapipi amesema mchujo huo utafanyika kwa lengo la kuepusha lawama kutoka kwa viongozi wa klabu na wachezaji kuhusu uteuzi wa wachezaji hao.

Wachezaji watakaofuzu zoezi hilo, wataondoka nchini Mei nne kuelekea China tayari kwa mafunzo hayo.