Jumanne , 25th Oct , 2016

Vilabu shiriki vya mashindano ya Taifa Cup mchezo wa Mpira wa Kikapu vimetakiwa kuhakiki mapema ushiriki wao ili kutoa nafasi kwa Shirikisho la Mpira wa Kikapu nchini TBF kuanza mapema mchakato wa kupanga ratiba ya michuano hiyo.

Moja ya pambano la katika mpira wa kikapu, Dar es Salaam

Kamishna wa Ufundi wa TBF Manase Zabroni amesema kwa upande wao kama shirikisho wameshajiandaa vizuri kwa ajili ya mashindano hayo yatakayoanza kutimua vumbi Novemba 17 mpaka 26 jijini Arusha na vilabu shiriki vinatakiwa kuthibitisha mapema kwani hawataruhusu klabu yoyote kuwasilisha uhakiki wake katika kituo cha mashindano huku akivitaka vilabu hivyo pia kufanya usajili kwa wakati.

Manase amewataka wadhamini pia kujitokeza kusaidia mashindano hayo kwani mashindano hayo yanalenga hasa kupata timu ya taifa hivyo misaada yao itasaidia hata kuweza kupata timu bora ya taifa itakayoiwakilisha nchi katika mashindano mbalimbali.