Ijumaa , 21st Nov , 2014

Mikoa mbalimbali nchini ambao ni wanachama wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa nchini BFT,imetakiwa kuwakilisha majina ya wawakilishi wa michuano hiyo itakayofanyika Desemba mosi mpaka tisa mwaka huu Viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es salaam.

Akizungumza na East Africa Radio,Katibu Mkuu wa BFT,Makore Mashaga amesema michuano hiyo yenye lengo la kutafuta timu ya taifa ya vijana itakayoshiriki michuano mbalimbali inatarajia kushirikisha vijana,watoto na wanawake katika mashindano hayo.

Mashaga amesema,pia watatumia mashindano hayo kama sehemu ya kumbukumbu ya aliyekuwa Baba wa Taifa wa Afrika Kusini Nelson Mandela aliyefariki Desemba tano mwaka jana.