Ijumaa , 4th Jul , 2014

Aliyekuwa mgombea wa urais wa klabu ya simba ya jijini DSM Michael Wambura leo ameutaka uongozi wa klabu ya hiyo kukaa na wanachama wake 69 iliyowasimamisha uanachama ili kumaliza mgogoro uliopo katika klabu hiyo.

Baadhi ya Wanachama na Mashabiki wa Klabu ya Simba wakiangalia moja kati ya mechi za timu hiyo.

Aliyekuwa mgombea wa urais wa klabu ya simba ya jijini DSM Michael Wambura leo ameutaka uongozi wa klabu ya hiyo kukaa na wanachama wake 69 iliyowasimamisha uanachama ili kumaliza mgogoro uliopo katika klabu hiyo.

Akizungumza jijini Dar es salaam leo, Wambura amesema uamuzi wa kuwasimamisha wanachama hao utachangia kuongezeka kwa migogoro katika klabu hiyo, na ili kufikia suluhu ni kuongea na wanachama hao na kuangalia suala zima lililopelekea wao kwenda mahakamani na siyo kuchukua hatua ambayo uongozi utaijutia baadae.

Wambura amesema kuwafungia wanachama hao ni hatua ya kinidhamu lakini ni uvunjifu wa haki za msingi hivyo itapelekea klabu hiyo kuwa na makundi ambayo yataongeza mgogoro utakaochangia kuvunja amani ya klabu hiyo na kupelekea uongozi kushindwa kusimamia timu na kutumia muda mwingi kutatua migogro na kusababisha timu kufanya vibaya katika mashindano mbali mbali