Michael Wambura akienda kuchukua fomu ya kuwania Urais ndani ya klabu ya Simba
Zoezi la uchukuaji na urejeshwaji wa fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya klabu ya soka ya Simba limezidi kushika kasi hii leo katika makao makuu ya klabu ya Simba maeneo ya msimbazi jijini Dar es salaam baada ya Michael Wambura kuchukua fomu hii leo.
Michael Wambura amejitokeza akiwa na maandamano ya umati wa watu kuchukua fomu za kugombea nafasi ya urais wa klabu hiyo, nafasi ambayo inawaniwa na mwanachama mwingine Evans Aveva ambaye yeye alirejesha fomu hii leo mda mfupi klabla ya Wambura kutua klabuni hapo.
Miongoni mwa watu waliorejesha fomu ni mgombea wa nafasi ya makamu wa Rais Swed Nkwabi.
Mbali na nafasi ya urais na makamu wa Rais lakini kivumbi kingine kipo katika nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo ambayo nayo inamshikemshike wa aina yake na mmoja wa waliochuakua fomu ni Colin Frisch.
Katibu msaidizi wa kamati ya uchaguzi wa Simba Khalid Kamguna amesema zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kuwania nafasi za uongozi wa klabu hiyo ambao uchaguzi wake utafanyika juni 29 mwaka huu litafungwa Jumatano jioni ya May 14 mwaka huu