Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Wallace Karia
Rais Karia ameyasema hayo Leo Septemba 19, 2022 wakati alipotembelea kambi ya timu ya Taifa Vijana U23 JMK Park Jijini Dar es Salaam inayojiandaa na mchezo wa kufuzu AFCON dhidi ya Sudan Kusini utakaochezwa Septemba 23.
''Watanzania wanamatumaini makubwa na nyie kwahiyo mkapambane muhakikishe tupata matokeo mazuri'' amesema Rais Karia.
Baada ya kusema hayo, Rais Karia amewataka vijana hao wacheze mchezo huo kwa juhudi kubwa ili kuhakikisha wanapata ushindi utakaosaidia kufuzu AFCON.