Jumanne , 22nd Dec , 2015

Baada ya kipigo cha 2-1 kutoka kwa Azam FC kocha msaidizi wa Majimaji Hassan Banyai amesema, hawajakata tamaa katika mbio za ubingwa wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara.

Banyai amesema bado wamo kwenye mbio za kuwania ubingwa wa msimu huu licha ya kufungwa.

Banyai amesema, tatizo linalochangia kupoteza katika katika michezo hiyo linatokana na wachezaji wake kukosa uzoefu na sasa atatumia muda mwingi kuwapa mbinu kwenye mazoezi yake kwa lengo la kuboresha kikosi hicho.

Banyai amesema kutokana na kiwango kizuri kilichooneshwa na wachezaji wake dhidi ya Azam FC ana amini watakuwa fiti katika mchezo utakaofuata dhidi ya wajela jela Tanzania Prisons utakaochezwa Jumamosi kwenye uwanja wao wa nyumbani.