Baadhi ya washindi wa tuzo mbalimbali waliokuwepo ukumbini wakiwa katika picha ya pamoja
Zimbwe amewashinda Aishi MANULA (Azam) na Saimon MSUVA (Yanga na ameondoka na kitita cha shilingi milioni 10.
Beki huyo ambaye amecheza michezo yote ya Simba ya ligi kuu msimu huu kwa dakika zote 90 kwa kila mchezo ametangazwa rasmi katika sherehe zilizofanyika usiku wa leo Mei 24, 2017 katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Mohamed Hussein
Mbali na tuzo hiyo ambayo ndiyo kubwa, tuzo nyingine zilizotolewa ni kama ifuatavyo...
Tuzo ya Goli Bora la Msimu inakwenda kwa Shiza Kichuya, bao alilofunga Feb. 25 katika mchezo wa marudiano dhidi ya Yanga. Kichuya, amewashinda Peter Mwarianzi na Zahoro Pazi
Tuzo ya Heshima inakwenda kwa Kitwana Manara mchezaji wa zamani wa Yanga na Taifa Stars aliyewika miaka ya 1960 hadi 1970
Mchezaji Bora Chipukizi ni Mbaraka Yusuph (Kagera Sugar), akiwashinda Shaaban IDD (Azam) Mohammed ISSA (Mtibwa)
Tuzo ya Ismail Khalfan (U-20) inakwenda kwa Shaaban IDD (Azam) akiwashinda Abdalah MASOUD (Azam) na Mosses KITAMBI (Simba)

Shaaban Idd akichukua tuzo yake
Mchezaji Bora wa Kigeni ni Haruna NIYONZIMA (Yanga), akiwashinda Method MWANJALE (Simba) na Yusuph NDIKUMANA (Mbao FC)
Tuzo ya Kipa Bora imekwenda kwa Aishi MANULA (Azam) akiwashinda Owen CHAIMA (Mbeya City) na Juma KASEJA (Kagera Sugar)
Tuzo ya Kocha Bora imekwenda kwa Mecky MEXIME (Kagera Sugar) akiwashinda Joseph OMOG (Simba) na Ettiene NDAYIRAGIJE (Mbao FC)
Tuzo ya mwamuzi bora imekwenda kwa Elly SASII (DSM) miaka 29, amewashinda Shomari LAWI (Kigoma) na Hance MABENA
Tuzo ya mfungaji bora imekwenda kwa Saimon Msuva (Yanga) na Abdulrahman Mussa (Ruvu Shooting), zawadi yao ni Tsh. mil 5.8

Saimon Msuva akikabidhiwa tuzo yake
KIKOSI BORA (4:4:2): Manula (Azam), Kimenya (Prisons), Tshabalala (Simba), Yakub (Azam), Mwanjale (Simba), Kenny Ally (Mbeya City), Msuva (Yanga), Niyonzima (Yanga), Abdulrahman Mussa (Ruvu Shooting), Mbaraka (Kagera Sugar), Kichuya (Simba)

Abdulrahma Mussa


