Jumamosi , 21st Jun , 2014

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) baada ya kupokea na kuzingatia maombi ya Simba, na kwa kuzingatia Ibara ya 26 ya Kanuni za Uchaguzi za TFF toleo la 2013 limeiruhusu klabu hiyo kuendelea na mchakato wa uchaguzi wao

Rais wa TFF Jamal Malinzi akizungumza katika moja ya mikutano yake na waandishi wa habari.

Rais wa shirikisho la soka nchini Tanzania TFF Jamal Malinzi amesema hali inayoendelea katika mchakato wa uchaguzi wa Simba ni masuala ya taratibu na kanuni za uchaguzi na kila mwanachama wa klabu hiyo ana haki kwa mujibu wa katiba ya klabu hiyo na kanuni za uchaguzi

Malinzi amesema kumekuwa na maneno mengi kuhusu yeye na mgombea aliyeenguliwa kuwania nafasi ya urais katika uchaguzi wa klabu ya Simba Michael Wambura kuwa anataka kumbeba mgombea huyo kitu ambacho si cha kweli

Aidha Malinzi amesema yeye hana maslahi yoyote na Simba na kitu anachokifanya sasa nikuhakikisha uchaguzi wa klabu hiyo unafanyika kama ulivyopanga na haki inatendeka kwa kila mgombea na hivyo TFF inawahimiza wanachama wa klabu ya Simba kuwa watulivu na wafanye uchaguzi wao Juni 29 mwaka huu kwa amani.