Jumatatu , 11th Jan , 2016

Naibu Waziri wa Habari,utamaduni,Sanaa na Michezo,Bi Annastazia Wambura,ametoa wiki moja kwa chama cha soka soka Wilaya ya Temeke TEFA kumtoa mwekezaji anayefanya shughuli za ujenzi kwenye uwanja wa mpira wa Tandika Mabatini jijini Dar Es Salaam.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Bi Annastazia Wambura, ametoa wiki moja kwa chama cha soka Wilaya ya Temeke TEFA kumtoa mwekezaji anayefanya shughuli za ujenzi kwenye uwanja wa mpira wa Tandika Mabatini jijini Dar es Salaam.

Mheshimiwa Wambura amesema hayo alipotembelea uwanja huo kukagua shughuli za ujenzi wa maduka zinazojengwa na uongozi wa chama cha soka Wilaya ya Temeke TEFA, lakini akashangaa kuona maandamano ya wananchi wakibeba mabango ya kutaka uwanja wao utumike kwa michezo.

Ndipo naibu waziri huyo alitaka maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa TEFA Peter Mhinzi kuhusu kinachoendelea.

Mwenyekiti wa TEFA alijitetea kwa kusema mwekezaji anashindwa kuendelea na ujenzi wa uwanja huo kwa sababu mahakamani kuna kesi iliyofunguliwa na wapangaji wa fremu za uwanja huo, wakipinga kupandishiwa kodi na kuvunjwa mkataba wao wa pango.

Ndipo Mh. Wambura akatoa agizo kuwa kwa kuwa Mahakamani kuna kesi kati ya wapangaji wa fremu za uwanja huo na TEFA, kitu kinachokwamisha ujenzi wa uwanja huo kwa muda mrefu, basi uanze kutumika mara moja na mwekezaji atoe vifaa vyake uwanjani hapo.

Akijibu agizo hilo mwenyekiti wa TEFA Peter Mhinzi amesema watamwambia mwekezaji huyo atoe vitu vyake ili uwanja huo uanze kwa shughuli za michezo.