Jumatatu , 17th Mar , 2014

Chama cha mchezo wa Chess Tanzania (TCA) kimesema hivi sasa kimeanza mchakato wa kuhakikisha mchezo wa chess unachezwa mashuleni.

Huo ni mpango mkakati wa chama hicho kuhakikisha mchezo huo unakua na kuenea kote nchini hasa kwa vijana wadogo walioko mashuleni.

Mwenyekiti wa (TCA) Geofray Mwanyika, amesema kuwa ili kufanikisha azma yao hiyo ni lazima waanzie na mafunzo kwa walimu walioko mashuleni.

Walimu hao kwa kushirikiana na baadhi ya wachezaji nguli wa mchezo huo, watafundisha katika mashule na ndio njia pekee ya kuueneza na kuukuza mchezo huo na hatimaye baadae nchi kupata wawakilishi bora katika medani ya kitaifa na kimataifa.