Ijumaa , 13th Mei , 2022

Mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs Heung-min Son sasa amefikisha magoli 21 ya ligi kuu ya England baada ya kufunga goli moja katika ushindi wa magoli 3 kwa 0 dhidi ya Arsenal usiku wa jana.

(Heung-min Son akishangilia goli kwenye mchezo dhidi ya Arsenal)

Son sasa yuko nafasi ya pili katika wachezaji wenye magoli mengi zaidi msimu huu akizidiwa goli moja na Mohammed Salah wa Liverpool mwenye magoli 22 na ndiye anayeongoza mbio za kuwania kiatu cha dhahabu cha ufungaji bora. Pia son ameweka rekodi ya kufunga idadi hiyo ya magoli pasipo mkwaju wa penati.

Mbali na goli hilo moja la Son katika mchezo huo, Harry Kane alifunga magoli mawili na kurudisha matumaini ya kumaliza ligi katika nafasi ya 4 kwa Tottenham hotspur baada ya kufikisha alama 65 wakiwa nafasi ya 5, na hivyo kuwa na tofauti ya alama moja tu na washika mitutu hao wa London wenye alama 66 wakiwa nafasi ya 4 ikiwa imebaki michezo miwili ligi kumalizika.

Arsenal wamebakisha michezo dhidi ya Newcastle United ugenini na Everton katika uwanja wa nyumbani, Huku Spurs akibakisha michezo dhidi ya Burnley wakiwa nyumbani na Norwich city wakiwa ugenini.