Alhamisi , 15th Dec , 2016

Klabu ya Simba imetangaza marekebisho madogo ya usajili iliyoyafanya katika dirisha dogo la usajili lililofungwa leo ambapo imewaacha rasmi Golikipa mua-Ivory Coast Vicent Agban na kiungo kutoka Kongo Mussa Ndusha.

Vincent Angban golikipa aliyeachwa

Taarifa ya klabu hiyo iliyotolewa vya vyombo vya habari imeeleza kuwa mabadiliko hayo ni kutokana na mapendekezo ya benchi la ufundi chini ya kocha Mkuu Joseph Omog

Taarifa hiyo pia imethibitisha Simba kuwasajili wachezaji raia wa Ghana, kipa Daniel Agyei na kiungo James Kotei, huku ikikamilisha taratibu za usajili kwa washambuliaji Pastory Athanas kutoka Stand United na Juma Luizio anayejiunga nayo kwa mkopo toka Zesco ya Zambia.

Katika maboresho hayo klabu imewapandisha wachezaji wawili wa kikosi cha vijana, Beki Vicent Costa na nahodha wa kikosi hicho mshambuliaji Moses Kitandu.

 

Sambamba na hao, klabu imewapeleka kwa mkopo Awadh Juma na Malika Ndeule kwenye Timu ya Mwadui FC ya Shinyanga, pamoja na Emmanuel Semwanza atakayekwenda Majimaji FC ya Songea,

Halikadhalika klabu imemrejesha Ame Alli kwenye timu yake ya Azam ambayo ilimleta ilikuwa imempeleka kwa mkopo.

Timu timu hiyo imeondoka asubuhi hii kuelekea Mtwara kwa ajili ya mchezo wa kwanza mzunguko wa pili dhidi ya Ndanda Fc, mchezo utakaopigwa siku ya Jumapili ya tarehe 18/12/2016 mjini Mtwara.

Wachezaji wa Simba wakisikiliza maelekezo kutoka kwa kocha wao Joseph Omog

Tags: