
Kauli ya umoja na ushirikiano huo umetolewa na kwa pamoja baina ya pande mbili yaani uongozi wa Simba chini ya Rais wake Evance Aveva na mwakilishi wa baraza la udhamini Mzee Hamis Kilomoni
Katika mkutano wao na wanahabari leo, kwanza Aveva anazungumzia juu ya kuwarejesha kundini wanachama waliofutwa na mkutano mkuu klabu hiyo mwaka jana akiwapa sharti la kufuta kesi waliyoifungua mahakamani ili waweze kukidhi vigezo vya kuwa wanachama
Wakati huo huo Baraza la udhamini wa klabu ya Simba limetoa hadhari kwa mtu yeyote atakayetaka kudhamini klabu hiyo ama kuwa kiongozi wa klabu hiyo atambue kuwa mali za klabu hiyo zitabaki kuwa za klabu chini ya baraza la udhamini.
Mwakilishi wa baraza la wadhamini Mzee Hamis Kilomoni amesema udhamini au aina yoyote ya mfumo wa uongozi kamwe hautakiwi kuingilia masuala la mali za klabu hiyo.
Mzee Hamis Kilomoni akizungumza sambamba na Rais wa Simba, Evance Aveva
Rais Aveva amesema, wanachama hao walifukuzwa uanachama mwaka 2014 mara baada ya kukiuka katiba ya klabu kwa kupeleka masuala ya mpira mahakamani na amekuwa akizungumza nao mara kwa mara kuhusu suala hilo ambapo amewataka kuiondoa kesi hiyo mahakamani na kuimaliza ndani ya Klabu.
Wakati huohuo Aveva amesema hali ya sintofahamu iliyokuwepo ndani ya klabu hiyo kati ya uongozi wa utendaji kazi uliopo madarakani hivi sasa pamoja na baraza la wadhamini la klabu hiyo hivi sasa wameshaimaliza na wanaendelea na kazi kwa maendeleao ya klabu.