Ijumaa , 24th Jun , 2016

Timu ya soka ya Vijana ya Shelisheli, imewasili Dar es Salaam saa 7.45 usiku wa kuamkia leo kwa ajili ya mchezo dhidi ya timu ya Taifa ya Vijana ‘Serengeti Boys’ utakaofanyika Juni 26 mwaka huu uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Kikosi cha Serengeti Boys

Kikosi cha Shelisheli kimeingia kikiwa na wachezaji pamoja na viongozi 25 kwa ujumla wake.

Waamuzi wanne kutoka Ethiopia, ndio watakaochezesha mchezo huo ambao ni Belay Tadesse Asserese ambaye ni mwamuzi wa kati wakati wasaidizi wake ni Tigle Gizaw Belachew upande wa kulia na Kinfe Yilma Kinfe upande wa kushoto huku mwamuzi wa akiba atakuwa Lemma Nigussie ambapo Kamishna wa mchezo huo atakuwa ni Bester Kalombo.

Mchezo huo ni wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17.