Rufaa ya Leeds United yakataliwa

Jumatano , 15th Sep , 2021

Chama cha Soka cha Uingereza (FA) kimetupilia mbali rufaa ya klabu ya Leeds United dhidi ya mchezaji wao pascal Struijks, alioneshwa kwenye mechi dhidi ya Liverpool baada ya kumfanyia madhambi Harvey Elliott.

Kiungo wa Liverpool, Harvey Elliot akionekana kwenye matukio tofauti tofauti baada ya kukwatulia na kiungo wa Leeds United, Paschal Struijik na kupekelea kifundo cha mguu cha Elliot kuteguka ba kumfanya Paschal kuoneshwa kadi nyekundu.

Struijks alitolewa nje ya uwanja, baada ya kumjeruhi kifundo cha mguu, kinda huyo mwenye umri wa miaka 18, aliyelazimika kuacha mchezo akiwa amebebwa kwenye machela kuelekea hospitali.

Elliot anatazamiwa kurejea uwanjani msimu hii ni kwa mujibu wa madaktari wa majogoo wa jiji wa Liverpool, huku Struijks akipewa adhabu ya kukosa michezo mitatu.

Mechi atakazokosa ni dhidi ya Newcastle united, Fulham (kombe la ligi) pamoja na mechi ya West ham United.