Pochettino amesema tunapaswa kukua kama timu pamoja na sio kwa mtu binafsi maana kwa aina hii ya uchezaji tunapaswa kushindana na kushinda michezo kwa kuwa mchezo wa soka ni kushinda ndio maana tunahuzunishwa na hali mbaya tunayopitia kwa sasa.
Chelsea inashika nafasi ya 14 kwenye msimamo wa EPL wakishinda mchezo 1 pekee kwenye michezo 6 na kuwa msimu mbaya zaidi kwao tangu mwaka 1978 huku jumatano Septemba 27-2023 watacheza na Brighton& Hove Albion kwenye kombe la Carabao Cup