Alhamisi , 7th Mar , 2019

Klabu ya soka ya Manchester United jana usiku imefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa, Ulaya kwa kushinda magoli 3-1 ugenini dhidi ya PSG.

Ole Gunnar Solskjær

Ushindi huo uliifanya Manchester United kufuzu kwa goli la ugenini baada ya matokeo ya jumla kuwa 3-3 kufuatia kukubali kichapo cha magoli 2-0 nyumbani kwenye mechi ya kwanza wiki mbili zilizopita.

Mabao ya Man United jana yalifungwa na Romelu Lukaku dakika ya pili na 30 kipindi cha kwanza, huku bao pekee la PSG Juan Bernat dakika ya 12.

Kwa upande mwingine katika mchezo huo mwamuzi Damir Skomina raia wa Slovenia, alimwamuru kocha wa Machester United Ole Gunnar Solskjær kuvaa BIB kwasababu nguo zake nyeusi ambazo alizivaa kufanana na jezi za PSG hivyo kumchanganya mwamuzi wa pembeni.

Mwamuzi wa pembeni wa upande wa pili, muda mwingi alikuwa anatembea kwenye 'touchline'karibu naye hivyo akaamuliwa kuvaa 'Bib' ili kuepusha usumbufu huo hususani kwenye maamuzi ya offside.