Niliwaaminisha uchawi - Ivo

Friday , 19th May , 2017

Golikipa mkongwe nchini Ivo Mapunda amefunguka na kusema wakati yupo nchini Kenya aliwaaminisha wapinzani wake kuhusu uchawi kupitia taulo lake ambalo mara nyingi anaingia nalo uwanjani.

Ivo Mapunda anasema ilifika wakati watu waliamini kuwa taulo analoingia nalo uwanjani linawazuia kufunga, kutokona na ushirikina na kusema imani hiyo ililetwa na aliyewahi kuwa mchezaji wa Yanga 

"Ni kweli issue ya taulo ilileta shida sana Kenya na hii inatokana na hii ilitokana na jinsi watu wanavyoamini ushirikina, ushirikana kwa Afrika Mashariki upo japo Kenya si sana ulinganisha na hapa kwa hiyo wakati nilikuwa natumia lile taulo, kuna mchezaji mmoja ambaye alikuwa akicheza hapa Tanzania alikuwa akicheza Yanga, alikuwa anaitwa John Baraza amecheza muda mrefu hapa kwa hiyo alikuwa ameingia kwenye yale mambo ya kishirikina. Nakumbuka ilikuwa mechi ya Sofapaka na Gor Mahia ambayo ndiyo ilileta shida, wakati mimi natumia lile taulo kujifutafuta, mbwembwe yeye akawa ameingiza zile imani" alisema Ivo Mapunda 

Mbali na hilo Ivo Mapunda alizidi kusimulia 

"Yule mchezaji aliwaambia wachezaji wenzake waje kwenye lile taulo walitoe kwa sababu anasema yeye anawajua Watanzania ni washirikina, kweli walichukua lile taulo wakatupa mimi nikalifuata nikalirudisha, wakatupa tena nikaenda kwa refa kulalamika refa akasema walirudishe, kwa hiyo hata mechi zingine nilizocheza bado waliamini hivyo wao walikuwa wanaamini lile ni 'magic taulo' hivyo nilipoona wachezaji wote na karibu timu zote zinaamini hivyo na mimi nikawaamisha, kwa hiyo kila nilipokwenda kwenye mechi nilikuwa nafanya mbwembwe zilezile kuwafanya waanze kufikiria taulo na si mchezo husika, lakini lile taulo lilikuwa halina kitu chochote" alisisitiza Ivo Mapunda