Alhamisi , 19th Jan , 2023

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amemtetea mshambuliaji wake Erling Haaland kutokana na kutofunga kwenye mechi za karibuni akisema kuwa wengi wanasahau haraka ubora waliokuwa nao.

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola

"Sisi tuna mchezo wetu, na tuna misingi yetu ya kucheza lakini jinsi tulivyocheza michezo miwili iliyopita haijamsaidia Haaland kufunga. Ni kosa langu mimi, sikuwaelewesha namna ya kushambulia"

Kuhusu ubora wa timu yake, Pep amesema, "Watu hawakumbuki kuhusu rekodi yetu, namna gani tulikuwa bora. Nikifa watu watazungumza jinsi Pep alivyokuwa bora, huo ndiyo ukweli"

Manchester City inakutana na Tottenham leo kwenye Ligi Kuu ya England, ikiwa imetoka kupoteza mechi mbili mfululizo zilizopita, dhidi ya Southampton kwenye Carabao Cup na nyingine dhidi ya Man United kwenye ligi.