Jumamosi , 18th Jun , 2016

Shirikisho la mpira wa meza Duniani ITTF kwa kushirikiana na chama cha mchezo huo nchini TTTA wameandaa kozi ya ukocha ngazi daraja la pili itakayofanyika jijini dar es salaam kuanzia Julai 04 mpaka 11 mwaka huu.

Kocha wa Timu ya taifa ya mpira wa meza Yahya Mungilwa amesema, kozi hiyo itashirikisha washiriki kutoka nchi za Nigeria, Falme za uarabuni, Kenya, Uganda na wenyeji Tanzania.

Mungilwa amesema, tayari Nigeria na falme za uarabu zimethibitisha kuleta makocha wao huku Kenya na Uganda wakiwa wameahidi kushiriki kozi hiyo huku bado wakiwa hawajathibitisha.

Mungilwa amesema, kwa upande wao kama TTTA wameshaandaa makocha wao 12 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania ili waweze kushiriki kozi hiyo ya kimataifa.

Mungilwa amesema, kozi hiyo itaambatana na kambi ya mafunzo kwa wachezaji wa timu ya Taifa ambayo itafanyika kwa siku mbili Julai 10 na 11mwaka huu.

Mungilwa amesema, baada ya kozi kumalizika, kambi hiyo ya wachezaji itaendelea ambapo makocha wa Tanzania wataendelea kuwafundisha wachezaji hao kwa muda watakaokuwa wamepangiwa na TTTA.