Jumapili , 27th Apr , 2014

Timu ya Taifa ya soka ya Tanzania kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 Ngorogoro Heroes hii leo imewapa raha watanzania kwa kuifunga timu ya Taifa ya Kenya kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 kwa penalt 4 kwa 3.

Baadhi ya Wachezaji wa Ngorongoro Heroes katika moja kati ya michezo yao, uwanja wa Taifa DSM

Timu ya Taifa ya soka ya Tanzania kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 Ngorogoro Heroes hii leo imewapa raha watanzania kwa kuifunga timu ya Taifa ya Kenya kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 kwa penalt 4 kwa 3.

Mechi hiyo ya marudiano ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 imechezwa leo Jumapili (Aprili 27 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ambapo Ngorongoro Heroes imeitupa nje ya kinyang'anyiro hicho timu hiyo ya kenya.

Hatua ya upigwaji wa “matuta” imefikiwa baada ya timu hizo kutoka suluhu ya bila kufungana katika dakika 90 za muda wa kawaida na ndipo mwamuzi alipoamua itumike njia ya Penalt tano kila upande, kuamua mshindi.

Wafungaji wa penalt hizo nne kwa upande wa Ngorongoro ni Mohamed Hussein “Shabalala”, Kelvin Friday, Mange Chagula na Idd Suleiman huku Mudathiri Yahaya akikosa baada ya mkwaju wake kupaa juu ya lango.

Kwa upande wa Kenya wafungaji ni Geofrey Shiveka, Timonah Wanyenyi na Victor Ndinya wakati Evans makari na Harison Nzivo wakikosa mikwaju yao.
 
Kwa matokeo haya sasa Ngorongoro Heroes iliyo chini ya kocha John Simkoko itacheza na Nigeria katika raundi itakayofuata.

Mechi ya leo imechezeshwa na waamuzi kutoka Burundi wakiongozwa na Pacifique Ndabihawenimana wakati Kamishna ni Tarig Atta Salih kutoka Sudan.

Kenya na Ngorongoro Heroes zilitoka suluhu katika mechi ya kwanza iliyochezwa Machakos wiki tatu zilizopita.