Jumamosi , 14th Dec , 2019

Klabu ya Yanga imeeleza masikitiko yake kufuatia kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la wazee wa klabu hiyo Ibrahim Akilimali.

Marehemu Ibrahim Akilimali enzi za uhai wake

Mzee Akilimali amefariki alfajiri ya leo Desemba 14, 2019 Bagamoyo Mkoani Pwani ambapo alikuwa akisumbuliwa na maradhi.

Ratiba ya mazishi itakuwa kesho Saa 10:00 jioni eneo la Tandale kwa Mtogole, jijini Dar es salaam.