Ijumaa , 21st Aug , 2015

WALIMU wa shule ya msingi Chokaa iliyopo wilayani Chunya mkoani Mbeya wapo hatarini kugongwa na nyoka wenye sumu kali aina ya koboko, kufuatia makazi yao kuwa mbali na shule hali inayopelekea kutembea umbali mrefu eneo la porini kuelekea shuleni.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Anyosisye Mwakisambwe amesema kuwa zaidi ya walimu 10 wamepanga mitaani kutokana na kukosekana kwa nyumba za walimu jirani na shule hiyo.

Amesema mara nyingi walimu wamekuwa wakipambana na nyoka aina ya koboko pindi wanapokuwa wakielekea shuleni kutokana na mazingira kuwa msituni.

Hata hivyo ameongeza kuwa tangu shule hiyo ianzishwe miaka 37, iliyopita imekuwa na changamoto ya barabara, maji, umeme na makazi ya walimu hali inayopelea kudumaa kwa kiwango cha taaluma.