Ijumaa , 15th Jan , 2016

Wachezaji wa Kimataifa wa Klabu ya Simba SC wametakiwa kujituma zaidi na kuhakikisha wanabadilika na ili kuisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi kuu bara.

Katika taarifa yake Kaimu Kocha Mkuu wa Simba, Jackson Mayanja, raia wa Uganda amesema, Simba inao uwezo wa kutwaa ubingwa licha ya kuonekana haina uwezo huo kwa sasa lakini kinachotakiwa kwa wachezaji ni kujituma ili kuweza kufikia malengo.

Mayanja amesema jukumu alilopewa ni kubwa la kuiongoza timu hiyo lakini tayari ameshaanza mikakati ya kukifumua kikosi kwa nia njema ya kuwaandaa wachezaji kisaikolojia ambapo lengo lake kubwa ni kuona kila mmoja anacheza kwa uwezo wake wote ili lengo la kutwaa ubingwa litimie.

Simba SC inatarajiwa kushuka dimbani hapo kesho kupambana na Mtimbwa Sugar katika muendelezo wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara.