Darren Earles mwenye miaka 52 ambaye alijiunga na klabu hiyo mwaka 2022 baada ya klabu hiyo kumilikiwa na taasisi ya uwekezaji ya Saudia Arabia ya PIF imetajwa ya kuwa ataendelea kuwa kwenye nafasi hiyo mpaka timu hiyo itakapo tangaza mtendaji mkuu mwingine.
Ijumaa , 27th Sep , 2024
Klabu ya Newcastle united imetangaza ya kuwa mtendaji mkuu wa timu hiyo Darren Earles atajiuluzu nafasi yake baada ya kugundulika kuwa na kansa ya damu ambayo imefikia hatua mbaya kiasi cha kuhitaji matibabu ya haraka ambayo kwa namna moja au nyingine yatakwamisha utendaji wake wa kazi.