Jumanne , 25th Oct , 2016

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho, amewataka wachezaji wake kuonyesha uanaume, na kusahau kipigo cha 4-0 walichofungwa na Chelsea, wakati huu, wakijiandaa na mchezo wa EFL Cup, dhidi ya Manchester City, kesho.

Jose Mourinho

 

Mchezo huo, wa kesho unawakutanisha tena makocha Mahasimu, Mourinho, na Pep Guardiola, wakati timu zao, zilipokutana katika mwezi wa Septemba na Manchester City kushinda 2-1 kwenye ligi ya EPL.

Mourinho, amesema wapo kwenye kipindi kigumu, sana, lakini watajitahidi kuishinda hali hiyo, baada ya kupoteza baadhi ya michezo ya ligi hivi karibuni.