Francis 'Chichi Mawe' Miyeyusho(aliyevua shati)
Francis Miyeyusho atapanda ulingoni Jumamosi hii kwenye ukumbi wa Karume ndani ya viwanja vya maonesho ya biashara vya mwalimu Nyerere kupambana na Ronald Pontillas wa Ufilipino.
Awali Francis Miyeyusho alinukuliwa akikataa kupigana katika pambano hilo kabla ya kubadilisha uamuzi wake na kutangaza kwamba atapanda ulingoni siku hiyo.