Jumatatu , 6th Jul , 2020

Mshambuliaji wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi anatarajia kumaliza kufanya kazi na maisha ya soka kwenye klabu ya Barcelona, amesema Rais wa klabu hiyo Josep Maria Bartomeu.

Lionel Messi

Bartomeu amekanusha ripoti zilizodai kuwa Muargentina huyo mwenye umri wa miaka 33, alikataa kuongeza mkataba wake unaomalizika mwaka 2021.

Bartomeu amesema kuwa moja ya wachezaji alioongea nao na kumthibitishia kuendelea kubaki Barcelona, ni pamoja na Lionel Messi.

Amezungumza hayo wakati timu yake ilipoondoka na ushindi wa 4-1 dhidi Villareal, Jumapili iliyopita, ushindi unaoifikisha Barca kwenye alama 73 nyuma ya vinara wa La Liga Real Madrid wenye alama 77, ikiwa imebaki michezo minne ligi kuhitimishwa.