Man United na Borussia Dortmund kuhusu Sancho

Jumamosi , 19th Jun , 2021

Klabu ya Manchester United imeongeza kiwango cha fedha ili ifanikishe kuinasa saini ya mshambuliaji Jadon Sancho ambaye kwasasa anakipiga katika Klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani.

Jadon Sancho akikipiga katika moja ya mchezo wa Bundesilga.

Inasadikika kwamba ofa ya awali ya Manchester United ya Pauni Milioni 67 ilikataliwa na sasa mashtani hao wekundu wameongeza hadi kufikia Pauni Milioni 77 ingawa Dortmund wao wanahitaji Pauni Milioni 85 ili imruhusu kinda huyo mwenye umri wa miaka 21.

Nyota huyo ambaye ana mkataba na Borussia Dortmund hadi 2023, amekuwa akiwindwa na Manchester United tangu msimu uliopita lakini klabu yake ilizuia kuondoka kwake kwa madai walikua na mahitaji yake.

Akiwa na Borussia Dortmund ,Sancho amehusika katika mabao 114 katika mechi 137 aliyocheza.