Alhamisi , 28th Sep , 2023

Ukiachana na kufanana kwa rangi ya jezi zao kwa maana rangi ya njano, Unaambiwa kwenye Ligi kuu ya nchini Afrika Kusini Klabu ya Mamelodi Sundowns imefanikiwa kuweka rekodi mpya ambayo pia imewahi kuwekwa na klabu ya Yanga.

Mamelodi Sundowns imefanikiwa kuweka rekodi mpya ya "UNBEATEN" baada ya kufikisha jumla ya mechi 32 bila kufungwa ikiwa ni rekodi ya mechi nyingi zaidi bila kupoteza kwenye historia ya Ligi kuu nchini humo, ambapo pia rekodi hii iliwahi kuwekwa na Yanga kwa kucheza mechi 49 bila kupoteza.