Ijumaa , 8th Jan , 2016

Mshambuliaji wa klabu ya soka ya Liverpool Jordon Ibe ataukosa mchezo wa leo wa kombe la FA dhidi

Mshambuliaji wa klabu ya soka ya Liverpool Jordon Ibe ataukosa mchezo wa leo wa kombe la FA dhidi ya Exeter City baada ya kupata majeruhi katika mechi iliyopita,

Ibe ambaye aliifungia bao la ushindi Liverpool dhidi ya Stoke city kwenye mechi ya mkondo wa kwanza wa kombe la ligi anaungana na wachezaji wengine saba wa kikosi cha kwanza cha klabu hiyo .

Kocha mkuu wa klabu hiyo Jurgen Klopp yupo kwenye wakati mgumu ikizingatiwa anamechi ngumu wikim ijayo ya ligi kuu ya soka nchini Uingereza dhidi ya vinara wa ligi hiyo klabu ya Arsenal.

Kwa ujumla majogoo hao wa Anfield wameshawakosa nyota wake 12 ambao wameumia wakiwemo Jordan Handerson,Philipe Coutinho ,Martin Skrtel,Kollo Toure na Dejan Lovren.