Jumapili , 6th Apr , 2014

Ligi ya klabu bingwa ya taifa ya kikapu inayoendelea katika uwanja wa ndani wa taifa jijini Dar es salaam imeendelea hii leo katika uwanja huo kwa michezo mbalilmbali kupigwa.

Moja kati ya michezo inayoendelea katika uwanja wa ndani wa Taifa

Ligi ya klabu bingwa ya taifa ya kikapu inayoendelea katika uwanja wa ndani wa taifa jijini Dar es salaam imeendelea hii leo katika uwanja huo kwa michezo mbalilmbali kupigwa.
Tumezungumza na mmoja wa waamuzi mahili katika michuano hiyo Haleluya Kavarambi ambaye amesema kuwa kozi za mara kwa mara kwa makocha na wachezaji kumesaidia kupunguza malalamiko juu ya maamuzi ya waamuzi mbalimbali katika michuano hiyo msimu huu
Kavarambi amesema ili kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa na kurekebisha yale makosa madogo ya kibinadamu wao kama waamuzi wamejiwekea utaratibu wakukutana kila baada ya mchezo na kujadili mapungufu na baadaye kuyafanyia kazi.
Na Miongoni mwa michezo iliyokua yakuvutia katika siku ya leo ni ule kati ya Tanga United iliyokwaana na Dodoma Wariours.