Akizungumza na East Africa Radio, mmoja wa mashabiki wa mchezo huo, Mopelle Mubarack amesema timu nyingi zimejitoa kutokana na kila mechi kuwa na ushindani kutokana na kila timu kujiandaa ambapo pia imepelekea timu kuongezeka katika mchezo huo.
Mubarack amesema wadhamini wanatakiwa kuendelea kujitokeza kwa wingi ili kuweza kuutangaza mchezo huu na kuweza kuukuza zaidi ndani na nje ya nchi.