
Ligi kuu ya soka Tanzania bara inaendelea tena kesho kwa michezo miwili itakayopigwa katika viwanja viwili tofauti ambapo mabingwa watetezi Yanga watakua ugenini kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, mjini Tabora kuumana na maafande wa Rhino Rangers
Mechi nyingine ni JKT Ruvu itakayokua mwenyeji wa Mbeya City katika mechi itakayochezwa katika uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni
Ambapo afisa habari wa TFF Boniface Wambura amesema kuwa bado TFF inaendelea na mchakato wa kurejea katika mfumo wa kutumia tiketi za kielektroniki
Na katika kuhakikisha wanakabiliana na mapungufu yaliyojitokeza wameunda kikosi kazi [task force] ambayo itahakikisha mapungufu yote yaliyojitokeza hayajirudii tena.
