Kocha Hans akimwaga wino, Singida United
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa klabu hiyo Abdulrahaman Salum Sima, imesema kuwa makubaliano na kocha huyo wa Kimataifa wa Uholanzi yamefikiwa leo Ijumaa tarehe 17, Machi, 2017 lengo likiwa ni kukata kiu ya mafanikio ya klabu hiyo.
Amesema mbali na kocha huyo, klabu hiyo pia imeingia makubaliano na kinda wa kimataifa Tafadwaza Kutinyu ambaye anacheza katika nafasi ya kiungo kutoka timu ya Chicken inayoshiriki Ligi Kuu ya Zimbabwe.

"Ni moja ya malengo makubwa ya klabu yetu kuona inasajili Kocha, wachezaji wazuri wenye sifa za kucheza michuano yote ya ndani na nje ya nchi yetu. Hivyo Kocha Hans ni hatua kubwa kwetu na tuna imani kuwa hii itaisogeza Singida United kwenye ramani ya soka barani Afrika na baadaye duniani kote” Amesema Katibu Mkuu Sima

