Kamati ya olimpiki Tanzania TOC imesema kamwe haitoingilia migogoro ya vyama vya michezo hasa pale linapofikia suala la uteuzi wa wachezaji watakaowakilisha vyama vyao katika michezo mbalimbali
Mwenyekiti wa kamati ya ufundi ya TOC Irine Mwakasanga amesema kuwa hivi sasa baadhi ya vyama vimekua vikivutana katika uteuzi wa wachezaji watakaoenda nje ya nchi kwa mafunzo ya maandalizi ya michuano ya madola
Aidha Mwakasanga ameongeza kuwa kinachoendelea katika chama cha judo ni kama siasa kitu ambacho si sahihi katika michezo, kwani tayari chama hicho kinafahamu kigezo cha mchezaji kufuzu ni kushinda dhahabu na hicho ndicho kitu ambacho TOC itakisimamia.