Kauli hiyo ameitoa kupitia ukurasa wake wa Twitter hii leo ikiwa ni siku moja imetimia kukiwa hakuna taarifa za kupatikana kwa mfanyabiashara huyo.
"Mashabiki wa Simba mko wengi sana. Bosi na mfadhili wenu mkuu ametekwa katika mazingira tata alfajiri, mpaka sasa mambo hayaeleweki . Ushauri wa bure, kama mpaka leo jioni 'MO' hatopatikana, ingieni mtaani nyumba kwa nyumba kufanya msako. 'People Power' haijawahi shindwa", amesema Mdee.
Taarifa kutoka kwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa inasema kuwa Jeshi hilo linaendelea na msako wa wahusika wa tukio hilo, ambalo limedaiwa kutekelezwa na raia wa kigeni.
Mohammed Dewji ni mwekezaji mwenye hisa asilimia 49 katika klabu ya Simba baada ya klabu hiyo kuridhia kuingia katika mfumo wa mabadiliko ya umiliki wa klabu, akiwekeza takribani Shilingi billioni 20.


