Alhamisi , 3rd Apr , 2014

Mchezaji wa mpira wa kikapu wa Tanzania, anayecheza ligi ya mpira wa kikapu nchini Marekani NBA, Hasheem Thabeet, ametoa msaada wa ujenzi wa uwanja wa mpira wa kikapu kwa shule ya kulea vipaji ya Lord Baden iliyoko mkoani pwani .

Hasheem Thabeet aliwakilishwa na mama yaek mzazi ambaye hii leo alikabidhi magoli mawili ikiwa ni mwanzo wa ujenzi huo na kusema kuwa ataendelea kumshawishi mwanae ili aendelee kusaidia michezo kwani ndio njia iliyomota hata yeye na kupata mafanikio aliyonayo sasa

Na kwa upande wake mkurungenzi wa shule hiyo ya vipaji kanali mstaafu Idd Kipingu ambaye ni mwalimu wa zamani wa Hasheem Thabeet wakati huo akisoama sekondari ya makongo amemshukuru Hasheem Thabeet kwa msaada huo na kuahidi kukamilisha ujenzi wake ukiwa na hadhi ya kimataifa.