Jumamosi , 3rd Jul , 2021

Bingwa wa Dunia wa kuendesha magari ya mashindano ya Langalanga, Lewis Hamilton amesaini Mkataba wa miaka miwili ya kuendelea kuitumikia Marcedes hadi mwaka 2023.

Bingwa wa Dunia wa mbio za magari, Lewis Hamilton akifurahia jambo.

Raia huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 36, ameshachukua ubingwa wa Dunia mara 7 tangu ajiunge na Marcedes mwaka 2012 akitokea McLaren.

Msimu huu, Hamilton anawania kufunja rekodi kwa kutwaa ubingwa wa Dunia kwa mara ya 8, ili ampiku Michael Schumacher lakini yupo nyuma ya dereva wa Red Bull Max Verstappen.

Awali Hamilton aligoma kusaini mkataba wa mwaka mmoja ambao ungemalizika mwaka 2021 akishinikiza kuboreshwa kwa baadhi ya vipengele vya mkataba lakini alisisitiza kuwa angeendelea kutumikia Marcedes.