Ijumaa , 18th Dec , 2015

Chama cha mchezo wa mpira wa magongo mkoa wa Dar es Salaam kimesema hakitakuwa na mashindano ya kufungia mwaka huu kama walivyopanga hapo awali ili kutoa nafasi kwa ajili ya mashindano ya mwakani.

Wachezaji wa timu ya Taifa ya Magongo wakiwa uwanjani katika moja ya mechi jijini Dar es salaam

Katibu mkuu wa chama hicho Mnonda Magani ameiambia East Africa Radio kuwa kwa sasa wanajipanga kwaajili ya mashindano ya klabu bingwa ya Taifa ya mpira wa magongo itakayoanza mapema mwakani jijini Dar es Salaam.

Magani amesema maandalizi ya michuano hiyo yamekamilika na timu zote zinatakiwa kuthibitisha kabla ya desemba 30 mwaka huu tayari kwa mashindano hayo ambayo pia watayatumia kuchagua wachezaji kwaajili ya timu za taifa.

hata hivyo kiongozi huyo amesema bado wanaomba sapoti kwa wadau ili waweze kutengeneza timu nzuri yenye ushindani itakayoiwakilisha Tanzania kwenye mashindano mbalimbali ya kimataifa.