Jumanne , 21st Oct , 2025

Awali hukumu ya rufaa hiyo ilipangwa kutolewa Septemba 25, 2025, kabla ya kuahirishwa kutokana na sababu za dharura.

Hukumu ya kesi ya rufaa iliyokatwa na Clinton Damas maarufu 'Nyundo' na wenzake watatu dhidi ya hukumu ya kifungo cha maisha gerezani inatarajiwa kutolewa leo Oktoba 21, 2025 na Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma.

Nyundo na wenzake ambao ni Askari Magereza C.1693 Praygod Mushi, Nickson Jackson maarufu Machuche, na Amin Lema anayejulikana kama Kindamba wamewasili ndani ya chumba cha Mahakama kusikiliza uamuzi huo.

Mawakili wa kujitegemea Godfrey Wasonga, Roberth Owino na Meshack Ngamando, wanauwakilisha upande wa kina Nyundo ambao wanajitetea huku upande wa Jamhuri ukiwakilishwa na Wakili Mkuu wa Serikali Lucy Uisso akisaidiana na mawakili wenzake wawili.

Haya yanajiri baada ya tukio la Septemba 30, 2024 lililoshuhudia Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma ikiwahukumu Nyundo na wenzake kifungo cha maisha gerezani baada ya kuwakuta na hatia ya makosa ya kubaka kwa kikundi na kumwingilia kinyume na maumbile binti mkazi wa Yombo, Dovya jijini Dar es Salaam, aliyetambulishwa Mahakamani kwa jina la XY.

Awali hukumu ya rufaa hiyo ilipangwa kutolewa Septemba 25, 2025, kabla ya kuahirishwa kutokana na sababu za dharura.