Jumamosi , 1st Aug , 2020

Dirisha la usajili kwa Klabu za Ligi Kuu , Ligi daraja la Kwanza , Ligi daraja la Pili na Ligi ya Wanawake limefunguliwa leo Agosti 1,2020.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi akizungumzia masuala mbali mbali yanayohusu Mashindano.

Klabu zitafanya usajili kwa muda wa mwezi mmoja ambapo dirisha litafunguwa Agosti 31 mwaka huu majira ya saa tano na dakika hamsini na tisa usiku.

 

Yeyote atakayejutana na changamoto kwenye mfumo wa usajili awasiliane na Idara ya Mashindano ya TFF.

TFF inasisitiza hakutakua na muda wa ziada ni vyema Klabu zikakamilisha usajili na uhamisho kwa wakati na muda uliopangwa.